Monday, November 28, 2011

GARY SPEED KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA WALES AJINYONGA.

                                          “there's no art to find the mind's construction in the face.” William Shakespeare

Gary Andrew Speed, amekutwa amejinyonga nyumbani kwake Cheshire, Speed ambaye alikuwa captain wa timu yake ya taifa ameyakuta mauti yake akiwa na umri wa miaka 42, Taarifa za kipolisi zinaeleza kuwa hakuna mazingira ya kutatanisha kuhusiana na kifo chake.
Speed alionekana kwa mara ya mwisho katika kipindi cha television cha BBC Football focus jumamosi na hakuonyesha dalili zozote kama ni mtu anayepanga kuondoa uhai wake baada ya masaa kadhaa, Speed ameacha mke na watoto wawili,
Inashangaza sana kwa Mtu kama yeye ambaye kila kitu kwenye maisha kilikuwa kinaenda vizuri na kwa mafanikio makubwa kuamua kuchukua uamuzi wa kujiua , huu ni uamuzi mkubwa na waajabu .RIP

No comments:

Post a Comment