Thursday, February 9, 2012

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2011,IN SUMMARY


Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Joyce Ndalichako alisema wasichana waliofaulu ni 90,885 sawa na asilimia 48.25 na wavulana ni 134,241 sawa na asilimia 57.51.

Wanafunzi 10 bora Kitaifa
Moses Andrew Swai kutoka shule ya Feza Boys,  Rosalyn  Tandau kutoka Marian Girls, Mboni Mumba kutoka St Francis Girls na  Sepiso Mwamelo kutoka St Francis Girls. Wengine na shule zao kwenye mabano ni  Uwella Rubuga (Marian Girls), Hellen Mpanduji (St Mary’s Mazinde Juu), Daniel Wallace Maugo (St Joseph Millennium), Benjamin Tilubuzya, (Thomas More Machrina), Simon Mbangalukela (St. Joseph Millennium) na Nimrod Rutatora (Feza Boys).

Wasichana 10 bora
Rosalyn (Marian Girls), Mboni  (St Francis Girls),  Sepiso Mwamelo (St Francis Girls),  Uwella Rubuga (Marian Girls) na Hellen Mpanduji (St Mary’s Mazinde Juu), (St Francis Girls Mbeya), Elizabeth Ng’imba (St Francis Girls Mbeya), Doris Noah (Kandoto Sayansi Girls),  Herieth Machunda  (St Francis Girls Mbeya) na Daisy Mugenyi (Kifungilo Girls Tanga).

Wavulana 10 bora  
Moses Andrew Swai (Feza Boys), Daniel Maugo (St Joseph Millennium), Benjamini Tilubuzya, (Thomas More Machrina), Simon Mbangalukela (St. Joseph Millenium) na Nimrod Rutatora (Feza Boys), Simon Mnyele (Feza Boys), Paschal Madukwa (Nyegezi Seminary), Henry Stanlay (St Joseph Millenium), Fransisco Kibasa (Mzumbe) na Tumain Charles (Iliboru).

Shule 10 bora 
Zenye zaidi ya watahiniwa 40: St. Francis Girls ya Mbeya, Feza Boys, St Joseph Millenium,  Marian Girls,  Don Bosco Seminary, Kasima Seminary,  St. Mary’s Mazinde Juu,  Canossa, Mzumbe na Kihaba.

Zenye watahiniwa chini ya 40: Thomas  More Machrina, Feza Girls, Dungunyi Seminary,  Maua Seminary,  Rubya Seminary, St Joseph Kilocha Seminary, Sengerema Seminary,  Lumumba,  Queen of Apostles- Ushirombo na Bihawana Junior Seminary.

Shule 10 za mwisho 
Zenye watahiniwa zaidi ya 40: Bwebwera, Pande Daraja, Mufindi, Zirai, Kasokala, Tongoni, Mofu, Mziwa, Maneromango na Kibuta.
Zenye watahiniwa chini ya 40: Ndongosi, St Luke, Igingwa, Kining’inila, Ndaoya,  Kilangali, Kikulyungu, Usunga, Mto bubu day na  Miguruwe.

Ubora wa ufaulu kwa jinsi  
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha kuwa, jumla ya watahiniwa 33,577 sawa na asilimia 9.98 wamefaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu.  “Wasichana waliofaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu ni 10,313 sawa na asilimia 7.13 na wavulana ni 23,267, sawa na asilimia 12.13,” alisema Dk Ndalichako.

Waliopata daraja la nne ni 146,639 sawa na asilimia 43.60 ambao wavulana ni  87,039 sawa na asilimia 45.40 na wasichana 59,600, sawa na asilimia 41.22.

Waliofeli ni 0156,089  sawa na asilimia 46.41, kati yao wavulana wakiwa 81,418 sawa na asilimia 42.47 na wasichana wakiwa 74,667, sawa na asilimia 51.64.

No comments:

Post a Comment