Thursday, November 10, 2011

Miss Tz part 1: Watanzania Tumechoka kuwa Wasindikizaji Miss World…

                                           Miss Tanzania 2011 Salha Israel
Hivi karibuni darbase.com ilikuwa ni mmoja ya mamilioni ya watu duniani ambao nilishuhudia mashindano ya Miss world yakitimiza miaka 60 na fainal zake kufanyika London Uingereza na Kama kawaida Tanzania tulipeleka Mwakilishi wetu Salha Izrael, na Kilichotokea ni kile ambacho tumekizoea na Mwakilishii wetu akabaki kuwa mshiriki na sio mshindani, ni hadithi ambayo imezoeleka,
Miss Venezuela, Ivian Lunasol Sarcos Colmenares,aliwashinda washiriki wengine kutoka nchi 113 na kutwaa taji hilo  baada ya kuwaridhisha majaji katika mashindano hayo kwa kufanya vizuri katika categories zote starting with beach beauty, top model, talent, sports, and beauty with a purpose - where the contestants must demonstrate involvement in a charity project.
Shindano la Miss Tanzania lina historia kubwa na inayovutia ambapo mshindi wa Kwanza kabisa anayetambulika alikuwa ni Bi Theresia Shayo ambaye alijinyakulia Taji hilo rasmi mwaka 1967, Shindano hilo lilipita kipindi cha kufungiwa na serikali mpaka mwaka 1994 pale akina Uncle Hashim Lundenga na kamati ya Miss Tanzania walipolifufua tena na kulijenga kulipa umaarufu mkubwa ulionao hivi sasa. Kuanzia mwaka huo ambako Aina Maeda alipata nafasi ya Kuiwakilisha Tanzania Miss world, Haijatokea mrembo wa Tanzania Kufanya vizuri katika mashindano ya dunia ukiondoa Mwaka 2005 ambapo mrembo Nancy Sumari aliweza Kunyakua taji la Miss Afrika kwa kufika Fainali ya top 7, darbase.com haitakuwa na fadhila kama haitotambua mafanikio mengi ambayo kamati ya Miss Tanzania imeyapata katika kipindi hicho, kubwa ikiwa ni kufanya Miss Tanzania kuwa shindano kubwa la urembo afrika mashariki na kati, uendeshaji wa ufanisi wa kamati pamoja na kufungua njia kwa warembo wengi ambao wamepata nafasi kupitia miss Tanzania, wengi wamepata kazi katika mashirika, wamefanikiwa katika fani ya modelling duniani na wamekuwa wakipewa zawadi ambazo zilianzia nyumba mpaka magari, ni mafanikio makubwa yanayostahili kuthaminiwa na wote wanaopenda maendeleo,darbase.com kama mdau wa urembo chini Tanzania inatoa pongezi kubwa kwa Hashim Lundenga na timu yake kwa mafanikio hayo
Miss Tanzania kutokana na mafanikio yake imeweza kuvutia Mashirika makubwa hapa nchini kutoa udhamini wa uhakika kitu ambacho wenzetu Kenya na Uganda hawajaweza kukifikia, Akina Lundenga na Timu yake wamefanya kazi kubwa, hili hakuna ubishi.
Kama ulipata nafasi ya kuangalia fainali za mwaka huu utagundua kuwa mashindano hayo yamebadilika sana, sio urembo pekee but it is beauty with purpose, Mashindano yamekuwa na vipengele vya beach beauty, top model, talent, sports, and beauty with a purpose - where the contestants must demonstrate involvement in a charity project.
Ukiangalia washiriki wa Nchi nyingine walivyojiandaa utaona kuwa sisi tunafanya mzahaa, Japo mrembo wetu alikuwa miongoni mwa walioingia fainali za Kipengele cha beauty with a purpose utagundua kuwa kazi yake ya siku moja tuu aliyoifanya hospital ya watoto haiwezi kufua dafu hata kidogo na kazi zilizoshinda za Miss Ghana Stephanie Karikari ambaye alipresent kazi yake ya ukarabati wa Kituo cha watoto yatima, pamoja na Miss Indonesia Astrid Ellena ambaye alionyesha kazi yake ya kuhudumia watu wenye matende zilikuwa ni kazi ambazo zinaonyesha ziliandaliwa vizuri na washiriki waliokuwa na wataalamu ambao wanajua ni nini cha kufanya ambacho kita katch judge emmotions and attention kila aliyeangalia zile clips aliguswa, na hii inatokana na maandalizi ya kutosha pamoja na kutumia wataalam.
 
Mashindano haya yamenifungua macho haswa pale nilipowaona washiriki wengine wakishiriki Midahalo katika Cambridge society, Topic zilizokuwa zinazungumziwa ni kuhusu masuala ya kijamii na dunia kwa ujumla, umahiri wa waliozungumza unaonyesha kuwa walishafanya hivyo huko makwao kabla ya kwenda fainali sidhani kama Salha wetu alipata hata nafasi kwenda kwenye jumuia za chuo kikuu hapa nyumbani kuzungumza na vijana masuala yanayowakaboli kama mtoa mada au mchangiaji kitu ambacho darbase.com tunaamini ni msingi mkuu kutayarisha kwa mashindano makubwa ya Miss world, hakika hakutayarishwa!
Washiriki toka Afrika kusini Bokang Montjane(Miss Africa) pamoja Miss Zimbabwe Malaika Mushandu na mshindi hawakunishangaza pale walipofika top 15 kwani kama ulipata nafasi kuangalia wakati wanaonyesha utamaduni wa kwao kwa ngoma lazima ukubali, walitayarishwa kwa mavazi ya asili pamoja na kuwa mahiri kuzicheza ngoma hizo. Hauwezi kuwa na utaalamu huo kwa kipindi kifupi tuu cha mwezi mmoja ni lazima walitumia muda mrefu kujiandaa.Inauzunisha Salha alishindwa hata kucheza sindimba loh.
Hili jambo linakera na kama lisipofanyiwa marekebisho tutakuwa wasindikizaji, hebu nasi tujifunze kwa wenzetu kama India, Afrika Kusini, hata alipotoka mshindi wa mwaka huu ambapo mshiriki wa mwaka huu alishinda taji hilo tangu mwaka Jana hivyo basi alikuwa na muda wa Zaidi ya mwaka kujiandaa. Kamati ya Miss Tanzania, wadau na wadhamini inabidi waangalie uwezekano wa kubadili ratiba ili mshindi wetu apate nafasi kubwa kujiandaa. Vilevile hii itasaidia mrembo kujiheshimu na kujilinda kwani kama ameshinda mwaka huu itambidi ashiriki fainali za mwaka ujao, na kama hatakuwa na maadili ni rahisi kumdhibiti kwa kumyima nafasi ya kushiriki fainali, ukomo wa muda wake uwe ni pale anaporudi Miss world, darbase.com inaamini nchi ya Venezuela itakuwa ni sehemu nzuri kujifunza kwani hii ni mara yao ya 6 kunyakua taji la miss world.
Nafikiri umefika wakati Kamati ya miss Tanzania kubadili mashindano ili yafanane na vipengele vinavyotumika Miss world, Washiriki ambao wanawakilisha mikoa / kanda kwenye mashindano ya Taifa ni Lazima wawe ni washiriki wazuri kwenye michezo, Kila Mshiriki ni Lazima awe amejihusisha moja kwa moja na Kazi za Kujitolea huko alikotoka na zaidi ya yote BASATA na serikali inabidi wakaze buti kuhakikisha kila mshiriki anajua japo kucheza ngoma moja ya kitamaduni ili atuwakilishe vyema; it is a matter of National pride, Kushiriki kazi za kijamii kutoka mikoani itaongeza credibility kwa shindano na washiriki na wazazi watakuwa na furaha kuona watoto wao wakijitolea moja kwa moja katika jamii yao. Ukiangalia washiriki wa mwaka huu zaidi ya nusu wanasoma vyuo vikuu na mmoja katika kila washiriki wanne ana elimu ya chuo kikuu. Basi na kwetu profile ya washiriki wa fainali za Miss Tanzania inabidi japo iwe na nusu ya washiriki wenye diploma, inawezekana!
Mshiriki wetu hakuandaliwa vizuri, jaribu kuangalia website ya Miss world uangalie her profile na za wengine mfano, Miss Kenya, Catherine Susan ANYANGO, Future ambitions? I would love to start a cancer foundation in Kenya.Favourite food? Pilau. Miss South Africa, Bokang Ramaredi MONTJANE .Future ambitions? To own a top arts and confidence school for girls in South Africa. To have my own talk show tackling social issues.  Favourite food? I love pap and tribe which is a traditional meat. Miss World, Venezuela, Ivian Lunasol SARCOS COLMENARES,Future ambitions ? Promote NGOs and work with children. Favourite food? My favourite food is chicken soup and the traditional pabellon of my country. Miss Tanzania, Salha Israel KIFAI, Future ambitions? To become a lawyer.Favourite food? My favourite food is Chinese pilau. Simlaumu Salha kwa kuwa na ambition za kuwa Lawyer katika shindano ambalo theme yake ni beauty with the purpose  na Simlaumu kwa Kupenda Chinese pilau na sio any other Tanzania traditional food kama makande,ugali dagaa n.k, kama washiriki wa nchi nyingine wanavyopenda vyakula vya kwao, hii imetokea   kwa sababu Salha hakuandaliwa, muda haukutosha!
La Mwisho nadhani sasa umefika muda wa Lino Agency kuweka utaratibu wa Kupanua wigo wa kuongeza na kubadili members wa kamati ya miss Tanzania, Damu mpya na mawazo mapya yanahitajika kutuvusha na kuleta mafanikio zaidi, Miss Tanzania ni shindano la Kitaifa na linahusu taifa zima lazima kuwe na watu wanaowakilisha makundi tofauti katika kamati ya miss Tanzania na wajumbe hao wasiwe wa Kudumu,Umefika muda kwa kamati ya Miss Tanzania to implement Salha motto  ‘Think Big, Dream Big, Achieve Big.’
Nawakilisha…Tony.for.www,darbase.com, wadau wa urembo na burudani nchini ,tell 0718-144 133   


3 comments:

  1. a word!!! inauma sana kila siku tu sisi tunasindikiza, mpaka lini? it a high time now wahusika wafanye mabadiliko, aibu!

    ReplyDelete
  2. Sisi huwa tunakurukupa mwisho na harakati za zima moto, huku tukiendekeza rushwa ya ngono na upendeleo. hatutafika popote kamwe

    ReplyDelete