Wednesday, January 4, 2012

WATANZANIA, SERIKALI HATUKUUTENDEA HAKI MLIMA KILIMANJARO.By darbase.com


Wakati Muheshimiwa waziri mkuu Mizengo Pinda akifunga kikao cha mwisho cha bunge mwaka 2011 mjini Dodoma pamoja na mambo mengi aliongea kwa masikitiko makubwa na kuelekeza lawama zake kwa vyombo vinavyohusika kwa ushiriki wao katika mchakato mzima wa ushiriki wa mlima Kilimanjaro kuwa ni moja wapo wa maajabu saba mapya ya dunia, hii inatokana  na Mlima Kilimanjaro kushindwa katika zoezi hilo mara baada ya kupata kura chache kulinganishwa na vivutio vingine vya Dunia vilivyokuwa katika mchakato huo.
Darbase.com kama wadau katika masuala yanaihusu jamii yetu ya Tanzania na taifa kwa ujumla imeguswa na kauli hiyo ya Waziri mkuu lakini zaidi tunaona kuwa sio tuu vyombo vya serikali vilivyotuangusha bali pia hata pia sekta binafsi na wananchi kwa ujumla wake hatukuutendea haki  mlima Kilimanjaro.
Ukiangalia kwa makini zoezi hilo ambapo mshindi aliamuliwa kwa kura atakazo pata sio ajabu kwa Mlima kimanjaro kushindwa na Table Mountain wa Africa kusini ambapo wao walionekana kujipanga vizuri huku wakiwatumia washindi wa tatu wa Tuzo ya Nobel, Askofu Tutu, Mzee Mandela na Frederick De Klerk katika kutafuta kura, huku Askofu Tutu akiwa ndio flag bearer katika matangazo ambayo yalirushwa ndani na nje ya Afrika Kusini,
 
“When God had created all there is, God said ‘Ahhhh’, I think I’ve got to do something special here. And so God produced this fantastic gateway in the south: Table Mountain, our mountain. What a wonder! Help us take our rightful place among the New7Wonders of Nature. My mountain! My vote!” 
 Ni wazi kuwa wenzetu walitambua kuwa kwa Kutumia kura za Afrika kusini pekee wasingeweza kushindana na vivutio kama Komodo kilichopo Indonesia, Iguazu Falls kilichopo katika nchi za Argentina na Brazil ambao walimtumia Lionel Messi star wa Barcelona na mchezaji bora wa Dunia ambaye alitengeneza video huku akitamka maneno yafuatayo “We need your vote to make Iguazu Falls win the World Cup of Nature Wonders. Vote for Iguazu Falls
 
 Halong Bay kilichopo Viet Nam , Amazon Kilichopo katika nchi za Bolivia, Brazil, Colombia, Ecuador, French Guiana, Guyana, Peru, Suriname naVenezuela. Si rahisi kwa kura za Watanzania pekee kushindana na Vivutio vilivyoko katika nchi hizi zilizo na idadi kubwa ya watu haiwezekani. Vyombo vinavyohusika vilikaa kimya wala hatukusikia vyombo hivyo kufanya juhudi za kupata kura Katika nchi zinazopakana  na Mlima kilimanjaro haswa Kenya kwa Kutumia spirit ya East Africa kwani hakuna asiye fahamu kuwa Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zinafaidika sana na Utalii kwa Kutumia kivutio cha mlima Kilimanjaro, Kwa Kutumia spiri ya East Africa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi pamoja na nchi nyingine rafiki kama Nigeria yenye idadi kubwa ya Watumia simu za Mkononi na internet zingetumika kuwahamisisha wananchi wa nchi hizo kuupigia kura Mlima Kilimanjaro
  
Inashangaza ni sababu zipi zilizowafanya wahusika kushindwa kuwatumia akina Dokta Salim Ahmed Salim and Dokta Asha Rose Migiro katika kufanya kazi hii ya ushawishi kama watanzania wenye kufahamika na kukubalika kimataifa,
Watanzania tumekosa ile hari na mwamko wa Utaifa tuliokuwa nao wakati wa Uongozi wa Baba wa Taifa, baada ya Kuona jahazi linaenda mrama hatukuchukua hatua yeyote kama raia tunayoipenda nchi yetu, hakukua na uhamasishaji katika mitandao ambao unahusisha makundi binafsi kama wanamazingira au hata friends of Kilimanjaro, mfano mzuri ni juhudi za Wanamazingira wa Indonesia baada ya kuona kuvutio chao hakipewi nguvu inayostahili na Serikali yao waliamua kuchukua jukumu hilo wakiongozwa na Emmy Hafild, Wanamazingira hao wa Indonesia  walitengeneza Kamati ya Kusuport Komodo Island na walifanikiwa kushawishi vyombo vya habari na hata Rais Susilo Bambang Yudhoyono na Mpinzani wake Kisiasa  Jusuf Kalla Kupiga debe kwa wananchi wa Indonesia  kwa kuupigia kura kivutio chao cha Komodo Island, Rais Yodhoyono  alitumia tukio la kufungua Uwanja mpya wa ndege wa Lombok International air port kwa kuupiga kura  kisiwa cha Komodo live on TV huku akiwataka mkewe na mawaziri wote kufanya hivyo mbele ya cameras na tukio hili kushuhudiwa nchi nzima, Masikini Mlima Kilimanjaro waziri mkuu alitumika dakika za lala salama huku watanzania wengi wakiwa hata hawaelewi ni nini kinachoendelea na pale makampuni ya simu za mikononi yalipokuja kuokoa jahazi kwa kuruhusu sms za bure ilikuwa ni sawa na kukumbuka shuka wakati tayari pameshakucha.
Katika Kampeni hizo kulionekana wazi kuna tatizo la jinsi gani ya kuwasiliana na jamii, Ujumbe uliokuwa unatolewa ni wa kijumla sana just vote for Mt kuingia maajabu saba ya Dunia, Kwa watanzania wa kawaida ujumbe huu unamuhamasisha vipi kutumia muda na pesa yake kidogo kupiga kura? Wenzetu kama Afrika kusini walitumia ujumbe huu wakimkariri Rais Mstaafu Nelson Mandela wakati akiwa kifungoni Robben Island, Nelson Mandela — who called Table Mountain “A Mountain of Hope”.
At the opening of the Table Mountain National Park in 1998, former president Mandela said: “During the many years of incarceration on Robben Island we often looked across Table Bay at the magnificent silhouette of Table Mountain. To us on Robben Island, Table Mountain was a beacon of hope. It represented the mainland to which we knew we would one day return.”
Hivi unataka kuniambia Mlima Kilimanjaro hauna  historia au any unique features? Jambo la ajabu mwaka huu ni mwaka ambapo tumetimiza miaka hamsini ya uhuru, na kumbukumbu zangu nakumbuka wakati wa matayarisho ya Tanganyika kupata Uhuru 1961 Baba wa Taifa alitembelea kambi ya Jeshi KAR, na kumpatia Mwenge wa Uhuru Marehemu Brigadier Nyirenda kuupandisha Mlima Kilimanjaro, Mwenge huo ilikuwa ni alama ya Umoja,Mwalimu alitamka maneno yafuatayo aliwahi kutamka maneno ”Sisi Tunataka kuwasha mwenge, na  Na kuuweka Kilimanjaro. Umulike hata nje ya mipaka yetu Ulete tumaini Pale ambapo hakuna matumaini…”

 Mashujaa wa uhuru wakati huo wakiongozwa na Nyirenda walipandisha mwenge huo na bendera ya Taifa mlima Kilimanjaro siku ya uhuru, Ilishindikana vipi kuwa na slogan ambayo ingewakilisha tukio hilo la kuwasha mwenge na kupandisha mlima Kilimanjaro siku ya uhuru Miaka hamsini iliyopita na Watanzania kuupigia kura mlima Kilimanjaro kuingia maajabu 7 mapya ya Dunia?
Kwa kumbukumbu zangu nakumbuka wakati Rais Kikwete anaingia madarakani moja wapo ya vitu alivyoanzisha ni Brand Tanzania, sijui ni taasisi au ni kamati sina hakika ninachoshangaa Brand Tanzania haikufanya lolote katika hili kwani kwa mtazamo wangu kama harakati za mlima Kilimajaro kuingia  katika maajabu mapya saba ya Dunia ni shughuli ambayo ilitakiwa kuratibiwa na Brand Tanzania, hii ni kwa sababu kunataasisi nyingi zinazohusika na mlima Kilimanjaro, Kuna KINAPA(Kimanjaro National Parks) TTB (Tanzania Tourist Boards, Wizara ya Mali ya Asili na Utalii,Pamoja na sekta binafsi. Brand Tanzania ingetumika katika kuratibu juhudi za serikali pamoja na sekta binafsi, Nauliuliza Brand Tanzania bado ipo? Wanafanya nini? Mbona sisi wengine Tunajua Brand Kenya,  ipo na Inafanya shughuli gani? Inasikitisha sana. Kuna haja ya kuangalia upya taasisi hiyo kwani kwa maoni yangu ni taasisi ambayo inabidi ichukue majukumu kama hayo kwa Sasa na Baadaye kwani suala la Uratibu lilikuwa ni tatizo katika kampeni ya milima Kilimanjaro kuingia maajabu saba mapya. Mungu ibariki Tanzania, Anthony “Tony” Gutta for www.darbase.com Tell 0713 144 133.
                                    

1 comment:

  1. It is a good article, hope the people and Institutions concerned will take notes for things to happen differently in future. We should remember those are just new 7 wonders of the world, some other time they will need to add new more and I strongly believe Tanzania will have something on the list. tujipange!! Keep it up bro!

    ReplyDelete