Friday, March 9, 2012

HII NDIO KAULI MPYA YA SERENGETI BREWERIES KUHUSU UDHAMINI WA TAIFA STARS

Kampuni ya bia ya Serengeti Brewers abayo imeidhamini Taifa stars toka mwaka 2007 imefunguka kuhusu kinachoendelea sasa kuhusu kusitisha kuidhamini timu hiyo.
Afisa uhusiano wa SBL amesema “sio kwamba imebwaga manyanga kuidhamini timu hiyo ila ni situation ambayo imejitokeza na kufanya hali ionekane hivyo japo tumeiweka kwenye ramani ya soka duniani kwa kuipeleka kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Brazil ili ijifunze”
Teddy amesema “hii ishu ya kuongezewa pesa ya kudhamini na TFF kwa asilimia 300 ni ya kweli, tumewaandikia TFF barua na tunasubiri majibu yao, mkataba wa kwanza tulianza kwa udhamini wa milioni 700 na mpaka mwaka jana ilikua imefikia bilioni 1.2 lakini sasa wanataka bilioni 3.6 ambayo itakua nyingi sana kwetu kwa mwaka ikizingatiwa kwamba ni lazima tusaini kwa miaka mitano ambayo ni zaidi ya bilioni 18, kama tutashindwa kuafikiana tutakwenda kuwekeza kwenye michezo mingine kama soka la beach na michezo mingine”
kwa kumalizia Teddy amesema “lazima tuangalie tunachotoa tutapata faida? kuanzia 2007 waliongeza asilimia 2, 3, 5 , 12 na tulikua tayari kwa mwaka huu watuongezee mpaka 15, 20 sio mbaya ila asilimia 300 ni kubwa sana na kama kuna mdhamini mwingine ambae ataweza kufanya hivyo itakua vizuri kwa soka la Tanzania”
TFF leo wamesema kwamba hawawezi kuitoa hiyo nafasi kwa kampuni nyingine mpaka watakapomalizana na SBL ambapo mazungumzo yao yamekaribia kumalizika japo kuna makampuni mengine ambayo tayari yamejitokeza kudhamini timu hiyo pamoja na kiwango kipya cha udhamini kilichotajwa.
Stori za chini chini sasa hivi ni kwamba kuna zengwe limetengenezwa ili kampuni nyingine kubwa iichukue hiyo nafasi ya SBL.

No comments:

Post a Comment