Monday, March 19, 2012

MJUE MTANZANIA ALIYETANGAZA KUJITOA FREEMASONS

Japokua anadai alikua mwanachama wa FREEMASONS, Samwel alikua anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya pia na amekiri kufanya biashara hiyo na baadhi ya viongozi wakubwa wa dini wa Tanzania na hata kukaa nao meza moja, hiyo alama kwenye sikio lake la kulia anasema waliwekewa kwa makusudi ili iwe rahisi kutambulika popote atakapotokea, yani ukimuona tu unajua huyu anauza hizo dawa za kulevya.

Hii ndio anasema ni alama kubwa aliyopigwa katika mgu wake wa kushoto kumtambulisha kwamba ni mwanachama wa FREEMASON, ni alama kama muhuri, iliyoambatana na KIAPO ambapo popote atakapokwenda atatambulika, amesema kwa sasa ndio inamsumbua sana kwa sababu chuma kilichotumika kumuwekea kimevunja mfupa, na hii aliifanya huko Afrika Kusini.

Samwel amesema alikimbia na kujiondoa kwenye dini hiyo inayodaiwa kuwa ya kishetani baada ya kutoka gerezani huko Afrika kusini, walikua wanatumwa kwenda kuua watu kwenye ajali na sehemu nyingine, walipewa irizi maalum ambapo baada ya kuona hayawezi hayo maisha akakimbia lakini mpaka sasa hivi anakiri kwamba anatafutwa kwa sababu ndio alikua anamalizia hatua ya mwisho kuingia kwenye hatua ya kutajirishwa kwa mali kama inavyotokea kwa waumini wengine, ila akatoroka na baadae ndio akasikia jamaa aliempeleka kwenye hiyo dini nae ameuwawa baada ya kugundulika kwamba alikua anataka kujiondoa.
Samwel anasema amewahi kwenda kwenye kanisa la FREEMASON hapa Dar es salaam Posta mara moja tu na kukutana na watu kadhaa maarufu wabongo ambao jumatatu ya march 19 2012 (kesho) kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM atawaongelea.
Samwel ametoa ushuhuda wake mwingine wa kuwepo kwenye hiyo dini ya kishetani kwenye NJIA PANDA ya CLOUDS FM.
CREDITS: Millardayo.com

3 comments:

  1. hii kiboko...sasa kama dio utawataja katika hicho kipindi si watakutoa roho wewe?!! tena viongozi wa dini mhhh. haya na tusubiri

    ReplyDelete
  2. huyu anajitafutia cheap popularity tu huyu hana lolote uongo mtupu. Tupa kule, freemason uwe wewe, usitudanganye, kafie mbali

    ReplyDelete
  3. we unataka uwd wewe! Kama huamini unyamaze au unapotosha kwakuwa nawe umo!

    ReplyDelete