Monday, April 2, 2012

MATOKEO YA UCHAGUZI UBUNGE ARUMERU, UDIWANI MWANZA NA MBEYA

Mbunge mteule wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasari asalimia wananchi wa Arumeru baada ya kutangazwa  kuwa mshindi asubuhi hii huko Arumeru

Matokeo ya kura za Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki yametangazwa  na Msimamizi wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi baada ya kupata kura 32,972 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CCM Bw Sioi Sumari aliyepata kura 26,757

Matokeo kwa Vyama vingine sita vilivyoshiriki ni kama ifuatavyoDP -77NRA - 35AFP - 139UPDB - 18TLP - 18SAU - 22

Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.


HUKO MWANZA NAKO... 

Wakati huo huo, habari kutoka Mwanza zinasema CHADEMA kimeshinda  katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kirumba mkoani  Mwanza.
 Msimamizi wa uchaguzi huo, Bw. Aloyce Mkono, amemtangaza kuwa mshindi mgombea wa Chadema Mh Dany Kahungu kwa kura 2,938 dhidi ya  mgombea wa CCM  Mh Jackson Masamaki aaliyepata kura 2,131.

Wagombea wengine walioshindwa vibaya katika uchaguzi  ni pamoja na Mh Haji Issa wa CUF aliyepata kura 184, Mh Kasala Muhana wa UDP amepata kura 7 na Mh Athuman Jumanne wa NCCR Mageuzi aliyeambulia 0 katika uchaguzi huo .Msimamizi huyo alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika katika hali ya amani na utulivu,na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na kuonyesha utulivu mkubwa wakati wa uchaguzi na zoezi la kutangazwa kwa matokeo.

HUKO MBEYA NAKO……….

Zoezi la uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kiwira mkoani Mbeya limekamilika usiku wa jana kwa wananchi kushiriki kwa amani uchaguzi huo ambao umemwezesha mgombea wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Laurent Mwakaribule kuibuka na ushindi wa kura 2621 kati ya kura 1649 alizopata mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM).

Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi mdogo wa kata ya Kiwila msimamizi wa uchaguzi huo Lauden Nnala alisema kuwa Chadema ndio washindi wa uchaguzi huo huku CCM ikishika nafasi ya pili na NCCR MAGEUZI wakishika nafasi ya tatu kwa mgombea wake kupata kura 33 huku chama cha wananchi (CUF) wakiambulia kura 13 pekee.

1 comment:

  1. CCM waombee asifariki mbunge au diwani wao kwani ikitokea watapoteza nafasi hizo katika uchaguzi mdogo, CHADEMA kwa sasa wanakubalika sana.

    ReplyDelete