Monday, April 2, 2012

WABUNIFU wa mavazi watatu watanzania washiriki onesho la wiki ya mavazi Afrika Kusini

Watanzania waliojitokeza kuhudhuria onesho hilo wakiwa wamepozi mbele ya camera    
Mwanamitindo Anastazia Gura akipita  mbele ya watamaji wakati akionesha nguo iliyobuniwa na mbunifu Jamira
Mwanamitindo wa kitanzania Bernad Chizi aliyechaguliwa kuonesha mavazi ya lebo ya House of Ole akipita mbele ya wahudhuriaji.  Wageni mbalimbali walihudhuria kuangalia onesho hilo.

WABUNIFU wa mavazi watatu watanzania wanaoshiriki onesho la wiki ya mavazi Afrika Kusini wametia fola katika onesho hilo. Wabunifu hao walishiriki onesho hilo kufuatia mwaliko wa mwanamitindo mahiri Millen Magese ambapo walionesha katika shoo iliyoitwa Tanzania International Fashion Exposition (TIFEX). 

Click the link below to read More




Wahudhuriaji waliofika kuona shoo ya watanzania hao walikuwa wengi na walivutiwa zaidi na namna ambavyo walichanganya kitenge katika kupendezesha mavazi yao. Mbunifu Evelyn Rugemalila ndie alifungua pazia kwa kuonesha mavazi yake aliyoyanakshi kwa kanga, aliweza kuzikonga nyoyo za washabiki na kujikuta wakimpigia makofi mara alipomaliza shoo yake.

Kitu ambacho alikifanya tofauti na wabunifu wengine ni wakati anamalizia shoo yake alitembea jukwaani akiwa amewavalisha sare ya nguo za kanga iliyofanana na yake huku. Baada ya Evelyin kuonesha ilifika zamu ya mbunifu wa mavazi Jamila Swai kuonesha mavazi yake ambapo aliongozana na mbunifu wa mikoba kutoka mradi wa Fahari wa Zanzibar Julie Lawrence.

Wanamitindo wa kizungu na kiafrika wakiongozwa na mwanamitindo mahiri nchini  Millen Magese waliwakilisha vema ambapo kila alipokuwa akitokea Millen watu walishangilia. Baada ya Jamila alifuata Doreen Noni aliwakilisha lebo yake ya Eskado Bird alifuata ambapo naye alitumia viashiria vya kanga pamoja na ngozi ngozi katika nguo zake.

Kwa pamoja wabunifu wa Tanzania walifanya vema katika onesho hilo huku wanamitindo nao wakiwa wamejitaidi kuonesha umahiri katika kutembea.

No comments:

Post a Comment