Thursday, April 12, 2012

shukurani na mwaliko wa kuenzi maisha ya hayati jane mponzi


Familia ya Eng. Gabriel Mponzi wa Oyster Bay, Dar es salaam,  na familia ya marehemu Dr.Allan Makange wa Kibaha, Pwani, zinapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa wote walioshirikiana nao kwa namna moja au nyingine kwenye kipindi kigumu cha msiba na kuhitimisha safari ya mwisho ya mpendwa wao Jane Mkami Mponzi.

Ni vigumu kutaja mtu mmoja kuwa ndiye aliyekuwa na msaada zaidi, ila hatuna budi kutoa shukrani zetu kwa madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Aga Khan kwa jitihada zao za kuokoa maisha ya Jane. Maparoko na mapadre wa kanisa katoliki la Mt. Petro Oyster Bay, Dar es Salaam pamoja na wale wa Ipamba Iringa na wanakijiji wake wote. Jumuiya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ya Oyster Bay Dar Es Salaam; IPP Media; Vodacom Tanzania; Africa Media Group; wamiliki wa blog mbalimbali Tanzania; majirani na marafiki zetu wote, asanteni sana.

Shukrani yetu kubwa ni kwa Mungu Mwenyezi kwa kutupatia zawadi ya maisha ya Jane hapa duniani, na tutaishangilia zawadi hii kwa kumsifu na kumtukuza Mungu siku zote za maisha yetu.

Tunapenda kuwakaribisha wote kwenye mkesha maalum wa kuyaenzi maisha ya Jane tarehe 13 Aprili 2012 kuanzia saa 11 jioni nyumbani kwa Eng.Mponzi #39, Br. Msasani, Oyster Bay. Pia kutakuwa na Misa ya shukrani kwenye kanisa la Mt. Petro Oyster Bay siku ya Jumamosi 14 Aprili kuanzia saa 12.30 asubuhi na baadae tutamalizia na chai nyumbani Oyster Bay. Wote mnakaribishwa sana. 


“Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi, Bwana Yesu kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake” Wafilipi 3:20-21 

No comments:

Post a Comment