Hii ni meli inayofanana kabisa na meli ya MV. Scagate iliyozama jana mchana kwenye kisiwa cha Chumbe |
Tanzania
imepata pigo linguine tena kwa vyombo vya usafiri wa majini ikiwa kufuatia kwa
ajali ya Meli ya Mv Stargate (Skagit) iliyotokea jana. Meli hiyo hiyo
iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar ilizama majira ya saa nane
mchana katika maeneo Pungume na Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.
Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana ilipindukia upande mmoja na abiria wengi waliweza kuokolewa kwa jitihada mbali mbali ikiwa ni pamoja na msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, MV KMKM, Tug ya Bandari na vyombo vyengine. Maiti kadhaa zilikwishapatikana na kiasi cha abiria 150 wameokolewa na waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Taarifa zinaeleza kwamba kulikuwa na watoto takriban 30 na Watalii kutoka nchi mbali mbali wafikao kumi.

Eneo la kisiwa cha Chumbe ambapo ajali ndio ilipotokea |
Baadhi ya abiria wakiwa wamekaa juu ya mgongo wa meli iliyozama wakisubiri kuokolewa |
Baadhi ya abiria wakisubiri kuokolewa |
Kila mtu alishika anapoweza bora kuokoa nafsi yake.. hawa walikamatia boya wakisubiri uokozi |
Ni moja ya baadhi ya meli zilizohusika kutoa mssada wa uokoaji |
Helikopta nazo hazikuwa nyuma kuhakikisha jitihada za uokoaji zinatekelezeka |
Mmoja wa waokoaji akiw ana maiti |
Waokoaji wakiwa wanaopoa mwili wa mmoja wa waliopoteza maisha |
No comments:
Post a Comment