Thursday, April 19, 2012

TAHADHALI KWA madereva WANAWAKE!

HABARI MDAU HASA MWANAMKE,NALETA TAHADHALI KWA WANAWAKE WAENDESHAO MAGARI,MIMI ILINITOKEA NILIENDA SHELI MAENEO YA VICTORIA NIKITOKEA MAKUMBUSHO MAJIRA YA JIONI,NIKAONA MADAM NAELEKEA MBALI NIKAJAZE UPEPO, NIKAENDA KWANZA PALE OILCOM NIKAFIKA PALE NIKAMWONYESHA YULE KAKA TAIRI MOJA LA MBELE NA SIKUSHUKA, MATOKEO YAKE KUJAZA UPEPO ALITUMIA MUDA MWINGI NIKAMUULIZA KULIKONI MUDA WOTE AKADAI OOH PAMPU MBOVU NIKAMWAMBIA BASI NAENDA PENGINE AKADAI OOH HUTAFIKA NIKAMUULIZA KWANINI?AKANIJIBU HAKUNA UPEPO NIKAMWELEZA MBONA UPEPO ULIKUWEPO IKANIBIDI NISHUKE KUSEMA UKWELI NINA KAWAIDA KABLA SIJAONDOKA LAZIMA NICHEKI MATAILI NA NILICHEKI KABLA SIJAWASHA GARI!NILIKUTA KAUTOA WOTE NA AKISISITIZA UTAFIKA POPOTE!NILIMJIBU UMEUTOA UPEPO NA SIJATOKA MBALI KWASABABU NILIKUWA NAWAHI NIKALIONDOSHA KWENDA SHELI YA VICTORIA ,FUNDI WA PALE AKASEMA DADA MBONA WAMETOA VALI KATIKA TAILI YAKO?KWELI NILISONONEKA SANA KUONA WATANZANIA TUMEKUWA WANYAMA KIASI HICHO!WALINIJAZIA NA KUNIWEKEA TENA VALI NA WALINIDAI 4,000/= NIKAWALIPA WALE WAKAKA WALIOKUWA WAMEVAA NGUO ZA BLUE!

NILIRUDI KUMUULIZA NA NILIPOFIKA AJABU NILIKUTA HIYO PUMP WALIOSEMA MBOVU WAKAWA WANAJAZA PRADO ALIKUWA ANAENDESHA MKAKA!NIKAMWELEZA NJAA ITAKUUA AKAJIFANYA KUWA MKALI NA AKAWA ANATETEWA NA WENZAKE KWASABABU NILIKUWA MWENYEWE NA MWENYEZI MUNGU HAJANIPA KIPAJI CHA KUONGEA NILIONDOKA LAKINI NIMEONA BORA NIWASAIDIE WANAWAKE WENZANGU WAJUE!KWELI NASIKITIKIKA SANA TENA SANA!NA SIJUI WALIKUWA NA MAANA GANI KWANI HATA NAKUMBUKA SANA ALINISIMAMISHA NA KUSISITIZA HUFIKI MBALI!NA ALIKUWA AKIWASILIANA NA WENZAKEWAMESABABISHA RING YA GARI YANGU IMEPINDA INABIDI NITAFUTE PESA YA KUNUNUA UPYA.NIMETOA ANGALIZO HILI ILI KINA MAMA MUONDESHAO MAGARI MUWE MAKINI UKITAKA KUWEKEWA UPEPO NAOMBA MUWE MNASHUKA!MSIKAE KAMA MIMI NILIKAA MANA SIKUANGALIA KINACHOENDELEA NA MUWE MAKINI NA HIYO SHELI!

No comments:

Post a Comment