Diamond akiwa Clinic ya Haemada jana |
Diamond akiwa anafanyiwa kipimo cha kifua |
Hali ya afya ya Msanii nguli wa Bongo Flava, Nassib Abdul ilitetereka hapo jana kutokana na kuugua na kukimbizwa hospitali. Haya chini ni maelezo ambayo Diamond aliyatoa kwenye Website yakekuhusian an ahali ya afya yake.
"Kiukweli hali yangu ilikuwa mbay asana, nilizidiwa na homa kali iliyosababishwa na kifua kilichonisumbua kwa wiki mbili mfululizo.. hadi kupelekwa Heameda Medical Clinic kwa Dr. Hery M. Mwandelelo ambaye ni Mtaalamu wa mambo ya Moyo na Kifua kwa ajili ya uchunguzi na vipimo vikubwa zaidi maana hali ilikuwa si ya kawaida. Namshukuru Mungu baada ya uchunguzi iligundulika kuwa ni kifua tu cha kawaida ambacho kilisababishwa na Tour za mfululizo ambazo nilizifanya bila kupumzika katika mikoa mbalimbali na nchi jirani. Kwa sasa naendelea vizuri na ninawashukuru wote mlioweza kuniombea kupitia mitandao mbalimbali kama blogs, Twitter, Facebook, Bbm, bila kusahau Media zote ili niweze kurudia afya yangu."
Darbase blog inakutakia nafuu ya haraka ili uweze kusimama tena imara kiafya na kuendelea kutupa burudani.
No comments:
Post a Comment