Friday, October 12, 2012

Waislamu wazua kitimtim Mbagala Kizuiani muda huu



HAPA NINAPOANDIKA HIVI NI KUWA MABOMU YA MACHOZI YANARINDIMA HUKO MBAGARA KIZUIANI ILI KUWASAMBARATISHA WAISLAMU AMBAO WAMEANDAMAMNA NA KUKIZUNGUKA KITUO CHA POLISI WAKITAKA KITUO HICHO KIMUACHIE KIJANA WA FORM ONE AMBAYE AMEKOJOLEA KITABU KITUKUFU CHA DINI HIYO YAANI MSAHAFU.

INASEMEKENA KIJANA HUYO ALIAMUA KUFANYA HIVYO BAADA YA KUTOKEA MABISHANO KATI YA YEYE NA MWENZIE KUWA UKIKOJOLEA KITABU HICHO UTAKUWA MWENDAWAZIMU LAKINI YEYE ALIPINGA NA KUAMUA KUKUKOJLEA MSAHAFU AHAKIKISHE KAMA NI KWELI ATAKUWA MWENDAWAZIMU AMA TOFAUTI. BAADA YA KUUKPJOLEA MSAHAFU HUYO KIJANA ALIYEKUWA NAE ILIBIDI AWAFAHAMISHE WAISLAMU JUU YA KITENDO ALICHOFANYA MWENZAKE.

JAMANI HAYA MAMBO YA IMANI NI MAGUMU MNO, SASA BASI KWANINI KILA MMOJA ASIAMINI TU ANACHOKITAKA BILA KUKASHIFU CHA MWENZIO. MFANO TU PALE MWENGE KITUONI SIKU HIZI WAMEANZISHA MIJADALA YA DINI YA KIISLAMU NA WAKIRISTO KILA UPANDE UKITOA AYA ZA KITABU CHAKE NA UPANDE MWINGINE UNAZUNGUMZA INACHOKIJUA JUU YA AYA HIZO. MAMBO HAYA YASIPOKATAZWA MAPEMA IKO SIKU PALE MWENGE WATU WATAPIGANA MIKWAJU NA MAJAMBIA.

No comments:

Post a Comment