Wednesday, October 10, 2012

Kesi ya Rama mla watu yendelea - apelekwa Mirembe

Kijana Ramadhani kulia akiwa na mama yake hapo katikati wote wakiwa chini ya ulinzi mahakamani
Mnamkumbuka huyu dogo Rama? ndio yulee alikamatwa kwenye geti la chuo kikuu cha muhimbili akiwa na kichwa cha mtoto mdogo wa miaka mitatu. msome zaidi hapa chini.



KIJANA aliyewahi kupata umaarufu mkubwa nchini kwa jina la Rama ‘mla watu’, Ramadhan Seleman anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji baada ya kukutwa na kichwa cha mtoto, Salome Yohana (3) mwaka 2008, amepelekwa Hospitali ya  Mirembe mkoani Dodoma, kupimwa akili.

Habari kutoka Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam zinasema kuwa mtuhumiwa huyo amepelekwa Mirembe ili kufanyiwa uchunguzi wa akili yake.

Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, afisa mmoja wa Jeshi la Magereza Kanda ya Dar es Salaam amesema wamelazimika kumpeleka Rama katika hospitali hiyo ya akili kutokana na vituko vyake.  
soma zaidi ....


“Tumeona ni heri tumfanyie uchunguzi wa akili kwa sababu ilikuwa ni vigumu kuendelea na kesi mahakamani kutokana na  vituko alivyokuwa akivifanya tangu alipokamatwa.

“Miongoni mwa mambo yanayotatanisha ni pale alipokamatwa akiwa anakula kichwa cha mtu, hicho siyo kitu cha kawaida, hivyo ni muhimu kumchunguza akili yake kwanza.

“Tukishabaini tatizo ndipo tutajua jinsi ya kuiendesha kesi hiyo inayomkabili,” alisema afisa huyo.

Ramadhan na mama yake Khadija Ally wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya mtoto Salome yaliyotokea Aprili 26, mwaka 2008. 

Mapema Oktoba  2011, Jaji wa Mahakamu Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Samuel Gibson Karua aliamuru mtuhumiwa huyo akapimwe  akili katika hositali hiyo.

No comments:

Post a Comment