Wednesday, November 2, 2011

ZITTO KABWE STATEMENT


Hii ni Taarifa maalumu ya Zitto Kabwe ambaye anaendelea na Matibabu nchini india, Zitto ambaye ni  mbunge wa kigoma kaskazini ambae pia ni naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni amezungumza kupitia ukurasa wake wa twitter.
Zitto kabwe amesema “Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika)
Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa Ijumaa octoba 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.
Baada ya hapo Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu na Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo alinieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni upasuaji na pale muhimbili hawafanyi hiyo operesheni Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.
Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya ‘dozi’ nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza dozi hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya opereshen.
napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya, sijafa na Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.
Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo, Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri- ZITTO KABWE

No comments:

Post a Comment