Sunday, April 15, 2012

washindi wa kili music awards 2012

Diamond and Ommy Dimples
Diamond ameendeleza ubabe katika fani ya Muziki wa bongo fleva baada ya kuibuka na Tuzo tatu katika vipendele vya  MTUNZI BORA WA MWAKA, MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME na Video yake ya Mawazo ikinyakua tuzo ya VIDEO BORA YA MWAKA na kuthibitisha kuwa yeye ni mfalme mpya wa bongofleva

Mbali na Diamond aliyebahatika kunyakua Tuzo mbili katika tuzo hizo ni msanii mwingine wa Bongo Fleva Suma Lee aliyenyakua tuzo za WIMBO BORA WA AFRO POP ambao alipata kupitia wimbo wa HAKUNAGA na Tuzo ya pili ni ya WIMBO BORA WA MWAKA ambao pia ni HAKUNAGA.

Aidha msanii Chiopukizi wa Bongo Fleva, Omy Dimpoz nae ametamba baada ya kunyakua tuzo ya WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA wa  NAI NAI aliomshirikisha ALI KIBA na pia alitwaa tuzo ya MSANII BORA ANAECHIPUKIA kupitia wimbo wake huo huo wa NAI NAI.

Nae Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani alikuwa katika kundi hilo la wasanii wenye tuzo mbili baada ya kupata tuzo ya WIMBO BORA WA HIP HOP wa  MATHEMATICS na Tuzo ya MSANII BORA WA HIP HOP.
Kwa List kamili ya washindi endelea kubofya hapo chini

1. WIMBO BORA WA RAGGAE.
-ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST.
2. WIMBO BORA WA DANCE HALL.
- MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN.
3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA.
- DUSHELELE BY ALI KIBA.
4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI.
- VIFUU UTUNDU BY A.T-
5. WIMBO BORA WA TAARABU.
- NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC ( AISHA MASHAUZI).
6. WIMBO BORA WA KISWAHILI.
- DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA-
7. WIMBO BORA WA AFRO POP.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-
8. WIMBO BORA WA R&B.
- NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL-
9. WIMBO BORA WA HIP HOP.
- MATHEMATICS BY ROMA-
10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
- OMMY DIMPOZ (NAI NAI SINGER).
11. RAPA BORA WA BAND.
- KALIJO KITOKOLOLO-
12. MSANII BORA WA HIP HOP.
- ROMA MKATOLIKI-
13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA.
 - NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA-
14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
-KIGEUGEU BY JAGUAR-
15. MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE.
- KHADIJA KOPA-
17. MTUNZI BORA WA MWAKA.
    - DIAMOND-
16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
- DIAMOND-
18. MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI.
- MANEKE-
19. VIDEO BORA YA MWAKA.
- MAWAZO BY DIAMOND-
20. WIMBO BORA WA MWAKA.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-
21. HALL OF FAME.
     -  TAASISI JKT-
22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
      - KING KIKII-
23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
     - DR. REMMY ONGALA-
24. MWIMBAJI BORA WA KIKE.
     - LADY JAY DEE-
25. MWIMBAJI BORA WA KIUME.
      - BARNABA-

No comments:

Post a Comment