|
Thika Highway - Kenya |
Tukubali tukatae jirani zetu hapo karibu na Mlima Kilimanjaro wanatuacha kwa kasi katika mambo mengi tu. Nikianglia pich ahiyo hapo juu ni moja ya barabara zao kubwa ambazo zimejengwa hivi karibuni. Hivi na sisi itawezekana kufika huku? hasa maeneo ya Bagamoyo road, Morogoro road, Pugu road, Kilwa Road... najua tukifika huku tatizo la foleni kwetu itakuwa hadithi za kale. ila sasa wananchi watakubali wavunjiwe majumba yao kupisha upanuzi wa barabara zetu? au ndio tutaandamana na kulala barabarani na kulaumu Mawaziri husika au serikali?
Hii ni ya pepmbeni tu, umesikia jana Raisi wao kagomea ongezeko la posho kwa wabunge wao? hay ana tusubiri kura za wabunge nazo zitasemaje maana nao wana nguvu sana....
No comments:
Post a Comment