BARAZA la Wazee la klabu ya Yanga ya
Dar es Salaam imeamua kuichukua timu ili kuiandaa na mechi dhidi ya wapinzani
wao wa jadi, Simba SC Mei 5, mwaka huu kufuatia mgogoro unaoendelea klabuni.
Asubuhi ya leo, wazee wa Yanga
wakiongozwa na Katibu wao Mkuu, Ibrahim Ally Akilimali walifika makuu ya klabu,
makutano ya mita ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kufanya Mkutano
na Waandishi wa Habari.
Katika Mkutano huo, Mzee Akilimali
alisema maamuzi hayo yana Baraka za Mwenyekiti wa klabu, Wakili Lloyd Baharagu
Nchunga.
Kwa sasa Yanga ipo katika mgogoro,
kufuatia Wajumbe wake wawili wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Abdallah Ahmed
Bin Kleb kujiuzulu kwa kutoridhishwa na mwenendo wa uongozi.
Machi mwaka jana, aliyekuwa Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Davis Mosha naye alijiuzulu kwa sababu za kutoelewana na
Mwenyekiti wake, Nchunga.
Yanga iliyopoteza matumaini hata ya
kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu, inaingia kwenye mechi dhidi ya watani
wa wa jadi, Simba walio katika hali nzuri.
Kwanza wana uhakika wa kuchukua
ubingwa na pili wanaendelea vizuri kwenye michuano ya Afrika, kesho wakicheza
mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al
Ahly Shandy ya Sudan
No comments:
Post a Comment