JUMA KILOWOKO- SAJUKI
Sajuki Hivi Ruge Mutahaba ni nani hadi watu wote
wamsikilize? Naamini kuwa ndio maswali mengi ambayo sisi wapenda majungu,
tusiona mazuri wala upendo akufanyiaye mtu mwingine wakati wa matatizo,
nimegundua kuwa chuki ujengwa na watu dhaifu na wabinafsi kutokana na uvuvi wao
pia kukosa ubunifu kwa yale wanayoyafanya katika jamii. Binadamu kama binadamu
ana mapungufu yake, lakini usimhukumu kwa sababu eti umemsikia mtu au jamaa
yako akimshutumu kama ni mtu mbaya na wewe kwa ujinga wako ukiendeleza chuki
maneno ya hovyo kwa sababu tu ya huyo aliyetengeneza uhasama huo, Ruge ndiye
mtu pekee ambaye ana uwezo wa kutoa msaada kwa kutumia kile alicho nacho,
lakini sisi ubaki na maneno yetu ya fitina na majungu tu na si kutoa hata kile
kidogo tulicho nacho. Najua wengi mtasema kuhusu makala hii lakini ukweli
unabaki pale pale kuwa Bongo watu kama Ruge ni wachache sana lakini kwa sasa
nahisi yupo peke yake tu, nimeshuhudia harakati zake nyingi sana akichangia
wananchi mfano mafuriko yaliyotokea Morogoro kule Kilosa ni yeye tu ndio
alibuni na kuratibu zoezi ambalo pengine nilitegemea wazo lile kufanywa na
Serikali au taasisi yoyote ya kijamii. Baada ya msiba wa nyota wa filamu
kutokea maneno mengi yalisikika kuhusu wizi wa michango ya fedha iliyotolewa
lakini wengi walimtuhumu Ruge kama mpigaji na kila sifa mbaya alitwishwa lakini
kwa sababu anatujua sisi Wabongo ambao maneno mengi bila vitendo alipotezea na
kukaa kimya lakini naamini kuwa hata katika nafsi yake alisema kuwa kumsaidia mtu
ni shida na lawama. Lakini nakumbuka kuwa Mwalimu wangu aliwahi kunieleza kuwa
hakuna msaada utolewao bure lazima utalipia tu iwe kwa kujua au kwa kutojua
kuwa umelipa au bado, hili si jambo la kusahau, linapotokea jambo linahitaji
utatuzi kwetu kidogo hatuwezi kufanya hivyo, basi inapotokea mtu kufanya ni
vema kumuunga mkono kuliko shutuma hilo limetokea na kuonyesha ni jinsi gani
kila msanii anahitaji kufa na tai yake shingoni. Waswahili usema kuwa Mungu
hamfichi mnafiki ikifika ndugu yetu Sajuki anaumwa na ilikuwa inatakiwa fedha
kwenda kutibiwa nje ya nchi yaani India, kila mwenye roho safi alitoa
alichokuwa nacho pia waandishi walijitahidi kuujulisha umma kama msanii huyo
anaumwa na anahitaji msaada wa matibabu, lakini michango ilikuwa ya kusuasua na
hata yale makundi yanasumbua Swahiliwood yaani Bongo Movie na TAFF yalichemka
kufanikisha. Nilifanya juhudi kwa kila njia ili mradi tu Sajuki aweze kusaidiwa
uelewa ulikuwa mdogo sana, tuliishia kumpigia simu tu huku tukimpa Sajuki
matumaini hewa bila upatikaji wa hizo fedha, hata pale walipofika viongozi wa
kiserikali nao bado walikuwa nyuma kuhusu maamuzi au njia ambayo ingetumika ili
kupata fedha. Kamati ziliundwa huku shutuma nazo zikitawala kila mtu akishidwa
kumwamini mwingine, hadi pale mgonjwa mwenye pamoja kuumwa alikata shauri na
kusema sisikii maneno majungu ya mtu nahitaji kumuona Ruge kwa msaada wangu ili
nipate kutibiwa, kweli alifanya juhudi hadi alionana na Ruge Sajuki anasema
kuwa alikaa na Ruge kwa muda mfupi alionyesha uwezo wake kubuni na kuratibu
tukio la kumwezesha kupata fedha. “Nilimweleza Ruge nimekuja ndugu yangu
unisaidie, nahitaji fedha kwa ajili ya matibabu na siku zinavyozidi kwenda ndio
naumia, hadi sasa naona ahadi tu ndio nyingi lakini hazina uhakika wa kupata
fedha, nilikuwa nikiongea huku nikiwa na mke wangu na rafiki yangu
Dino,”anasema Sajuki. Baada ya hapo ndipo Ruge alipomjibu kwa kusema kuwa
anaguswa na tatizo lake kwa sababu ameenda yeye atamsaidia kabla alifuatwa na
wasanii wengine lakini kutokana na wasanii kutokujitambua na kumuona kama yeye
ni mtu dhulumati ilimpasa kubaki kama mchangiaji mwingine tu ambaye angeweza
kutoa kiasi alicho nacho kwa upendo wake au kuguswa na tukio hilo. “Hivi sasa
tunawaogopa sana nyinyi wasanii walikuja wenzako na kuniomba lakini sikuwa tayari
kufanya lolote lakini kwa sababu umekuja mwenye sina budi kukusaidia na tukio
hilo linaanza kuanzia sasa lazima tujue tunapata hiyo fedha ya
matibabu,”alisema Ruge. Ruge alichofanya ni kubuni wazo haraka nalo lilikuwa
kutumia wimbo uliokuwepo katika filamu ya wasanii hawa yaani Sajuki na Wastara
kutoka katika filamu ya Mboni yangu kuimbwa na wasanii wapatao 27 wakijumlishwa
na Waheshimiwa Wabunge zoezi lilofanyika siku hiyo hiyo na kila mtu alitii wito
ikiwa ni Wabunge na wasanii wote hasa wa muziki kwanini Ruge asiitwe Shujaa wa
Maafa? Pamoja na hayo jambo lakusitikisha ni ushiriki wa wasanii wenye shughuli
kwa maana ya waigizaji ni wasanii wane tu ndio waliotia sauti katika wimbo wa
Mboni yangu ambao ni Wema Sepetu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na William Mtitu
sambamba na mhusika Wastara hiyo inaonyesha ni jinsi gani tulivyogawanyika
lakini siku ya siku tutakuwa wakwanza kusema Ruge kapiga hela tuache maneno
haya ya kuwachafua watu wakati sisi hatuwezi kitu. Ukisoma tu habari au
kusikiliza Redio hata Televisheni utagundua kuwa wasanii wana matabaka makubwa
ambayo hayawasaidii zaidi ya kuwatia umaskini tena wa kujitakia, Dina alisema
kuwa kuna na wasanii wa filamu ambao wamekuwa wakijitoa hata uwaite saa nane za
usiku watakuja ambao ni Mtitu, Wema na Shilole hili ni tatizo. Inawezekana kuna
wasanii hawakuja kwa sababu hawakupigiwa simu kutokana na uzito wao lakini pia
wadau hata kama wasanii ni wazito katika matukio ya kijamii tuwaite tu
wasipokuja lakini ujumbe wamepata, kwani nimeamua kumpongeza Ruge kwa kuwa
mbunifu hata mimi ungenipa Redio na Televisheni na kuniambia nifanye tukio
litalomshawishi mtu kuchangisha fedha kama hiyo bado ingekuwa kitendawili.
Tunajifunza nini kutokana na tukio la Sajuki? Bado
safari yetu ni ndefu sana kujikomboa kutoka mikononi mwa utumwa uliotuzingira
kwa sababu ya ubinafsi, wezi wanaodhulumu kazi zetu kwa bei nafuu kwa kununua
haki zetu hatuwaoni, ni kweli ilimpasa Sajuki kuingia location ili apate fedha
za matibabu? Kumbe wasanii hawakopesheki jambo linaloashiri mwisho mbaya. Ruge
Mutahaba mratibu wa zoezi la kumchangia Sajuki. Hatuwalaumu wasanii kwa kukosa
fedha bali kwa kukosa umoja na kujenga hoja au sera zinazoweza kuaminiwa na
kuonyesha thamani yenu kwa ajili ya kuwasaidia, mara nyingi usikika wasanii
wakishirikiana na watu maarufu au viongozi lakini hakuna msaada wa kudumu
nahisi kuwa hakuna mtu anayewa kutoa hoja na ukweli kuhusu maslahi ya jumla.
Leo hii katika tasnia ya filamu kuna taasisi mbili zinazohitaji kuongoza
wasanii kila unavyongea na upande mmoja kila mtu anajitahidi kumlamu mwenzake
wengi wanajiuliza malumbano haya ya Bongo Movie na TAFF ni lini yataisha na
kuwa wamoja watakaokaa na kujadili kwa kauli moja na kusema biashara ya filamu
iende hivi? Yaliyojitokeza katika msiba ni aibu kuyasema lakini ilikuwa doa
kubwa kulisafisha yahitaji muda sana maana tulishuhudia watu wakipiga picha au
kutawala uongozi huku hata mitafaruku ikiendelea chini kwa chini kama vile
kutengenezwa Beji zilizotaka kutambulisha pande moja bila sababu ya msingi,
lakini pia wasanii kugombana kutokana na makundi hayo ni aibu sana. Hivi ni
kweli unaweza kupendwa na mtu mwingine bila ya wewe kujipenda? Hili tumeliona
kwa Sajuki msanii anahitaji kupata fedha za matibabu lakini ilikuwa ni utata
hadi pale mtu anayelaumiwa kuingia na kufanya harambe, kwa wasanii kubuni kitu
chochote lakini haikutokea hivyo wasanii waliojitokeza ni watatu tu, duh,,,
Binadamu kama binadamu hayupo aliyekamilika kwa asilimia mia moja, lakini kama
kuna mtu anaweza kufanya kazi au tukio la kijamii apimwe kwa jambo hilo haina
maana kuwa wasanii wote hawajielewi bali kuna wachache wanaowapeleka wengine
shimoni, tujadili kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu Tanzania na wasanii
wake. CHANZO:www.filamucentral.co.tz hongera kwa mwandishi na filamu central
kwa makala hii
No comments:
Post a Comment