Monday, June 4, 2012

Meet Miss Akuot Philip Suzan Mrembo toka South Sudan, Atakayeiwakilisha nchi yake Mashindano ya Miss East Afrika 2012.



Mrembo huyo ni Miss Akuot Philip Suzan (20) mwenye urefu wa futi 6.1 anaekaa
Juba, Sudan ni mwanamitindo Nchini humo na anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha makerere Nchini Uganda mwaka huu.
Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika Nchi mbalimbali kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritrea: Miss Rahwa Afeworki (22), kutoka Ethiopia ni: Miss Lula Teklehaimanot (19) na Miss Ayisha Nagudi (23) ambae ni mwakilishi wa Uganda.
Nchi zilizobaki zinaendelea kutafuta wawakilishi watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ambayo yatazishirikisha Nchi 16 za ukanda huu ambazo ni Tanzania (wenyeji), Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine ni Southern Sudan, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia pamoja na visiwa vya Mauritius, Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.
Mashindano ya Miss East Africa ndiyo mashindano makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa ambazo huandaliwa na kumilikiwa na
Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam, Tanzania.

No comments:

Post a Comment