Thursday, July 26, 2012

Chameleon alalamikia kitendo cha kunyanganywa passport yake Tanzania

Chameleon akifanya vitu vyake kwenye tamasha la usiku wa Matumaini tar 7/7/2012 uwanja wa Taifa

Chameleon akifanya vitu vyake kwenye tamasha la usiku wa Matumaini tar 7/7/2012 uwanja wa Taifa

Lile saga la Passport kati ya C.E.O wa Global Publisher Eric Shigongo na mwanamuziki maarufu kutoka Uganda Josee Chamelion bado linaendelea baada  ya mwanamuziki huyo jana kuandika kwenye wall yake ya Facebook kulalamikia kitendo cha Mtanzania Eric Shingongo kukamatia Passport yake  kwa karibu mwezi sasa. Tukio la Shhigongo kukamata passport ya Mwanamuziki huyo lilitokea baada ya Shigongo kudai kutapeliwa $3,500 za malipo ya awali aliyodai kuyafanya kwa Meneja wa Chamelion. Kwa mujibu wa Chamelion mwenyewe ni kuwa aliyemtapeli pesa hizo sio Meneja wake bali ni tapeli  wa huko Uganda anayekwenda kwa jina la George. Mwanamuziki huyo aliandika kuomba ushauri kwa kitendo alichofanyiwa ambacho anadhani ameonewa. Angalia chini upate status ya Chameleon.



No comments:

Post a Comment