|
Hamis Kiiza akishangilia na wachezaji wenzie wa Yanga baada ya kufunga goli la pekee jana |
Mchezaji
Hamis Kiiza ya Yanga mwenye asili ya Uganda jana amefanikiwa kuipeleka timu
yake ya Dar Young African kwenye fainali ya kombe la Kagame kwa goli pekee
alilofunga kwenye mchezo huo katika kipindi cha nyongeza. Kiiza alifunga bao
hilo, kwa kichwa akiunganisha krosi ya karibu ya Haruna Niyonzima ambaye
alitumia mwanya wa mabeki wa APR kuzubaa wakisikilizia maamuzi ya refa, baada
ya Kiiza kuangushwa.
Yanga
waliinuka na wakaanzisha shambulizi la haraka lililozaa bao hilo. Dakika tatu
baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita alitolewa nje kwa kadi nyekundu
ya moja kwa moja na sasa ataikosa fainali.
Katika
Fainali hiyo ambayo intachezwa jumamosi katika uwanja wa Taifa Yanga watakutana
na Azam Fm amabo wlaipata nafasi hiyo kwa kuitoa timu ya Simba SC kwa kipigo
cha mabao 3-1 mwanzoni wiki hii. Mechi hii ambayo inatarajiwa kuwa katika mechi
ngumu katika kombe hili ambapo watani wa jadi wa Yanga Simba wakiwa wanaombea
watani wao wa Jadi kiwakute kile kilichowakuta wao kutoka kwa wababe hao Azam;
wakati tiku ya Yanga yenyewe ikiwa na kazi mbili tofauti, moja ya kutetea kombe
na ya pili kuonyesha kwamba hawako tayari kunywesha juice ya Vijoti kutoka kwa
wana Azam Fc
|
Kikosi cha Yanga kitakachopambana Jumamosi |
|
Kikosi cha Azamu kitakachopambana jumamosi |
more pictures after the cut...
|
Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao jana |
|
Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao jana |
No comments:
Post a Comment