Friday, July 27, 2012

NI NANI KUNYAKUWA KIATU CHA DHAHABU KAGAME CUP?


Bihanuzi akiwa amembeba Hamisi Kiiza
Mchecheto wa  je ni nani kunyakuwa kiatu cha dhahabu cha Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame umezidi kupamba moto baada ya John Raphael Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC na Hamisi Kiiza ‘Diego’ wa Yanga kutimiza mabao matano kila mmoja, hivyo kulingana na Said Bahanuzi ‘Spider Man’ anayeshika nafasi ya pili, nyuma ya Taddy Etikiama na AS Vita ya DRC, mwenye mabao sita.
Wachezaji wote hao wanne, watakuwa na fursa ya kuongeza mabao yao Jumamosi, Bocco, Kiiza na Bahanuzi wakicheza fainali kati ya Yanga na Azam, wakati Taddy akiiongoza AS Vita katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, dhidi ya APR ya Rwanda.    

John Bosco wa Azam Fc

Wengine waliomo kwenye kinyang’aniyo hicho ni Suleiman Ndikumana wa APR mwenye mabao mabao matatu, ambaye pia anaweza kuongeza mabao yake katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu keso.
Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC timu yake imetolewa akiwa ana mabao mawili sawa na Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA.

MSIMAMO WA MAGOLI ULIVYO:
Taddy Etikiama                 AS Vita        6
Said Bahanuzi                   Yanga SC     5
Hamisi Kiiza                     Yanga SC     5
John Bocco                       Azam FC    5
Suleiman Ndikumana       APR              3
Abdallah Juma                  Simba SC    2
Leonel St Preus                APR            2
Didier Kavumbagu           Atletico        2
Feni Ali                            URA           2
Robert Ssentongo             URA          2 

No comments:

Post a Comment