Thursday, July 19, 2012

JE WACHEZAJI WETU WANAWEZA KUFIKA HUKU KWELI?

Vanessa akiwa anaonyeshwa magari ya kifahari yanayomilikiwa na mchezaji mpira Adebayo.
 
Umepata kumsikia Sheyi Emmanuel Adebayor (aliyezaliwa tar. 9 Februari, 1985 mjini Lome, Togo)? Huyu ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Togo - mwenye asili ya Nigeria. Kwa sasa anaichezea klabu mashuhuri barani Ulaya ya Manchester City. Na pia huichezea Timu ya Taifa ya Togo.
Hivi karibuni mtangazaji mrembo wa MTV Base mwenye asili ya Kitanzania Vanessa Mdee alimtembelea nyumbani kwake na kupiga picha hizo akiwa katika matayarisho ya kipindi chake kitakachokwenda kwa jina la MTV Base meets with MTN ambacho kitaanza kuruka kuanzia tarehe 1 Agosti, 2012. Stay tuned!
Ukiangalia mafanikio ya Adebayo na ukilinganisha na hali ya wachezaji wetu kwa kweli tofauti ni kubwa sana na inasikitisha. Tatizo ni nini? Nini kifanyike na wakwetu wafike japo nusu ya hawa Waafrika wenzetu wanaosukuma kabumbu huko nchi za wenzetu? Je, inawezekana kweli kufika huku? Nani na nai wanahusika kufutikisha huku?
Adebayo na Vanesa Mdee wakiwa katika mazingira ya jumba la mcheza kabumbu huyo

Haya endelea kuona picha zaidi za mafanikio ya Mcheza kabumbu huyo.

Wakiwa ndani ya moja ya magari ya kifahari yanayomilikiwa na Adebayo

Vanessa akiwa mbele ya swimming pool katika jumba la kifahari la Adebayo


No comments:

Post a Comment