Mashabiki wa Simba, jana wamemtembezea kichapo mama mmoja (pichani juu) aliyekuwa
amevalia jezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), kosa kukaa kwenye jukwaa walilokuwa
wamekaa wao.
Sasa haikuweza kufahamika mara moja, mashabiki wa Simba wana bifu na TFF
au hawapendi timu ya taifa. Mama huyo alikimbizwa huku akipewa kichapo hadi
kutokwa damu, kabla ya kuokolewa na Polisi waliomteremsha jukwaani. Aliporwa
vitu vyake kama pochi na kadhalika.
Baadaye akiwa amekwishaokolewa na askari, ndipo msamaria mwema mmoja,
albino akamuokotea baadhi ya vitu na kuwakabidhi askari. Huwezi kulipa jina
lingine tukio lile, zaidi ya udhalilishaji wa kijinsia. Alikuwa anatia huruma
mama huyo wakati anahangaika kujitoa kwenye kundi la mashabiki wa kiuma wa
Simba, iliyofungwa 3-1 na Azam katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame. Chungulia hapo kupata picha zaidi ya tukio
No comments:
Post a Comment