Tuesday, July 31, 2012

Riziki popote .. Kutana na Konda Rehema Juma

Mwanadada Rehema Juma ambaye ni Konda kwenye bus la Mwenge Posta
Rehema akiwa busy kurudisha chenji za abiria wake.
 Darbase leo ilifanikiwa kukutana na Konda Mwanadada mstaarabu na mchapa kazi, mke wa mtu, mama wa watoto wawili Bi Rehema Juma ambaye ni Mkazi wa Magomeni Mapipa. Ni tofauti kama inavyodhaniwa na watu wengi kuwa kazi za ukonda ni za wanaume tu lakini sio kwa dada huyu yeye alionekana kufurahia kazi yake ambayo huwa anaianza asubuhi saa 11 na kumaliza saa 2 usiku ili aendelee na majukumu yake kama mama na mke mwema. Rehema aliiambia Darbase kuwa kazi yake hiyo anaithamini sana kwani kwa siku huwa inamuuigizia kipato cha shilingi 30,000/ mpaka 40,000/.

Darbase inamtakia kila la heri Bi Rehema kwa kazi yake hiyo na pia mfungo mwema maana wakati akiongea na sisi alikuwa kwenye swaum.

Tunaomba radhi kwa ubora wa picture ila tunaahidi kukuletea full coverage ya maisha ya Rehema, challenges anazopata kwneey kazi yake na Nice photoz of course.

No comments:

Post a Comment