Mwigizaji wa filamu nchini Stive Mangele 'Stive Nyerere jana alikuwa anakabidhi filamu yake ya Mwalimu Nyerere kwa Mama Maria Nyerere ikiwa kama shukrani zake, baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama. Stive alisema kwamba kumpa filamu hiyo ni kuweka kumbukumbu kwamba, anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi
Mama Maria Nyerere akionyesha filamu hizo alizokabidhiwa na Steve Nyerere
Amesema Mama Maria Nyerere alimsaidia
sana katika kumuonyesha vitu gani mwalimu alikuwa akifanya, na vitu
gani mwalimu alikuwa akivipenda, na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa
baada ya kazi zake. Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambapo
walijitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo ili
ikamilika.
No comments:
Post a Comment