Monday, September 10, 2012

Kakakuona aonekana Kilwa

Mnyama Kakakuona akiwa amewekewa viu mbalimbali ili achague kimoja ambacho hutoa ishara ya kutokea kwa kitu hicho hapo mbeleni
 Mnyama inayesemekana wa ajabu Kakakuona na ambaye huonekana kwa nadra sana ameonekana jana katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Mnyama huyo anapoonekana wanaomuelewa wanamuwekea vitu mbalimbali ikiwa kama kumtaka atabiri ni nini kitatokea kwa kipindi kijacho. kama akielekea kwenye maji wengi huwa wanadai ni mvua za kutosha. Jana katika vitu alivyowekewa mnyama huyo alielekea kwenye mtungi wa gesi na kuulambalamba ambapo kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo hayo ya imani wanadai kutakuwa na gesi ya kutosha maeneo hayo na hasa ukizingatia tayari maeneo hayo yashagunduliwa gesi na inasubiriwa tu kazi ya uchimbaji iendelee.
Sina uhakika sana kama haya mambo ni kweli au ni mambo tu ya Imani mbofumbofu!1 kam ani kweli basi nadhani kila nyumba bongo itaatumia gesi na kusahau mkaa; magari yote bongo tutatumia gesi na kuachana na Kiwese ambacho kinapanda bei kila kukicha.
more pictures after the cut


Kakakuona akiwa katika pozi

Kakakuona akiusogelea mtungi wa gesi

No comments:

Post a Comment