|
Katibu Mkuu wa Jukwaa la
Wahariri Bw. Neville Meena akizungumza mara baada ya waandishi wa habari
kumaliza maadamano yao ya Amani kutoa ujumbe wao kwa jeshi la Polisi kutokana
na kupoteza maisha kwa mwandishi wa habari Marehemu Daudi Mwangosi aliyeuwawa
katika vurugu kati ya Polisi na Wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) katika kijiji cha Nyololo Mkoani Iringa hivi karibuni, Maandamano
hayo yalianzia katika ofisi za kituo cha Televisheni ya Chanel Ten ambako
marehemu alikuwa mwakilishi wake mkoani Iringa na kuishia katika viwanja vya
Jangwani jijini Dar es salaam hapo jana.
|
|
Waandishi wa habari
mbalimbali wakitoa dukuduku zao mara baada ya kumalizika kwa maandamano hayoi.
|
|
wandishi wa habari Mkongwe Bw
Jackton Manyerere akizungumza katika maadamano hayo kwenye viwanja vya Jangwani
jijini Dar es salaam
|
|
Waandishi wa habari
mbalimbali wakiwa wamejikusanya katika ofisi za Chanel Ten kabla ya kuanza kwa
maandamano hayo.
|
|
Katibu Mkuu wa Jukwaa la
Wahariri Bw. Neville Meena akitoa ratiba ya njia ambazo maandamano yatapita
kabla ya kuanza kwa maandamano hayo wanaofuatia katika picha ni Profesa
Rwaitama, Jane Mihanji na Rashid Kejo.
|
|
Waandishi wa habari
wakiandamana huku wakiwa wamebeba picha ya marehemu Daudi Mwangosi
|
|
Maandamano yakiendelea
kupitia mitaa kadhaa jijini Dar es salaam
|
|
Hapa yakiwa yamefikia katika
barabara ya Morogoro kuelekea Jangwani.
|
|
Waandishi
wa habari wakiigiza vurugu zilizotokea mkoani Iringa ambapo Mwandishi wa
habari Marehemu Daudi Mwangosi alipoteza maisha katika vurugu hizo. |
|
Mdau Maximilian kutoka kituo
cha Televisheni cha Mlimani TV.
|
|
Polisi nao hawakubaki nyuma katika kuhakikisha kuwa swala zima la usalama linachukua mkondo wake |
Katika Maanadamano hayo yaliyooishia Viwanja vya Jangwani, Waandishi hao walikataa uwepo wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Nchimbi ambaye alikuwepo hapo kuyapokea maandamano hayo kwa sababu walizodai kuwa wanampenda mno lakn kwa siku ya jana hawakumuhitaji kwani hakuvaa vazi la wahusika waliokuwepo pale.
No comments:
Post a Comment