Monday, November 14, 2011

CHANNEL O AWARDS,SABABU ZILIZOMFANYA DBANJ ASHINDWE KUHUDHURIA


Dbanj msanii mwenye mafanikio makubwa Afrika na duniani aligoma kuhudhuria sherehe za tuzo za channel music video awards 2011 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuchukizwa na waandaaji kumpatia tiketi ya ndege economy ticket badala ya tiket ya Business Class ambayo inaendana na hadhi yake. D banj ambaye alitakiwa kupokea tuzo maalumu ya Special recognition award  alipania sana kuwepo katika shughuli hiyo lakini ilimbidi kuahirisha mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege tayari kwa safari na kugundua kuwa tiket aliyoandaliwa ni ya daraja la tatu(economy) kitu ambacho anaona hakiendani na hadhi yake aliyonayo

Dbanj alipiga u turn na kurejea nyumbani kutoka airport na kuwaacha waandaji wakijitahidi kuokoa jahazi na kuelekea makazi ya Dbanj lekki na kukubaliana kurekodi salam zake kwa wapenzi za kukubali kupokea tuzo yake.

Dbanj alikataa kupanda ndege kwa daraja hilo la chini kulinda hadhi aliyoitafuta kwa jasho kubwa, vipi wadau unamuunga mkono dbanj au?

No comments:

Post a Comment