Monday, January 23, 2012

JAMAA AAMUA KUMUOA GIRLFRIEND WAKE BAADA YA KUFARIKI



Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni!! Haya yametokea huko Thailand kwenye jimbo la Surin ambapo kijana aitwae Chandil Deffy aliamua kufunga ndoa na girlfriend wake wa miaka 10 aitwae Sarinya “Anne” Kamsook. Tukio hilo lilifanyika mbele ya ndugu na jamaa na bibi harusi alipelekwa mojamoja kuzikwa baada ya tukio la ndoa kama inavyojionyesha pichani. Wawili hao walikuwa na mipango ya kufunga ndoa kwa siku za usoni lakini lengo hilo halikutimia baada ya girlfriend huyo kufariki katika ajali na ndio sababu kubwa iliyomfanya Chadil kutimiza ahadi yake ya ndoa huku akiahindi kumpenda daima mpaka mwisho wa maisha yake.
Duuh, sasa sijui jamaa hatooa tena au?!!!

1 comment:

  1. ukisikia kudata sasa ndio huku. miaka yote kumii kashindwa kumuoa haya ndio kaja kumuoa maiti!!! as if she will know abt it..lol

    ReplyDelete