Saturday, July 28, 2012

NA MPIRA UMEKWISHAA... YANGA BINGWA KAGAME CUP 2012

Wachezaji wa Yanga wakiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa kombe lao jioni hii
 Ndani ya uwanja wa Taifa mechi kati ya Yanga FC na Azam FC imemelizika huku Ynaga ikiwa na ushindi wa magoli mawili kwa BUYU yaliyofungwa na Hamisa Kiiza dakika ya 44 na Said Bahanuzi dakika za nyongeza. kumalizika kwa mechi hiyo inamaanisha Yanga ya Dar es Salaam ndio bingwa wa Kagame Cup kwa mwaka huu. ongera Yanga kwa kundeleza  ubabe na kubakiza kombe la Kagame Jangwani.
Kiiza na Bahanuzi wote wana magoli sita ya kufunga mpaka mwisho wa kombe hili. je nani atapata kiatu cha dhahabu kati ya hao watatu wenye magoli sawa yaani 6 kila mmoja? Taddy Etikiama wa AS Vita ya Congo pia ana magoli 6.

Watani wa Jadi mpooo? semeni hongera basi hahah

No comments:

Post a Comment