Saturday, July 28, 2012

VIJANA WA UAMSHO DAR WAWAPA KICHAPO MACHANGU


vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona…
Vijana wa Kiislamu wenye Imani kali na wanaodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania bara wiki iliyopita walileta songombingo baada ya kuwatembezea bakora machangu au dada poa kwa kudai kitendo chao cha kuendelea kujiuza kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kuonyesha dharau kwa mwezi huo ambao watu wengi huwa wanauthamini na kuwa watulivu.
Safisha safisha hiyo ilianzia maeneo ya Barabara ya shekilango mpaka kituo cha mwenge ambapo kwney kila kituo cha daladala au mikusanyiko ya dada hao walisimamisha bajaji yao waliyokodi na kutembeza bakra ambapo kila dada hao walitimkia wanapopajua wao. Baada ya kumalizza zoezi hilo maeneo ya Sinza vijana hao walihamia maeneo ya Kinondoni ambapo pia biashara hiyo imeshamiri.
Hii safishasafisha campagn ilianzishwa baada ya usiku mmoja kina dada hao kumvamia muumini wa dini hiyo aliyekuwa anakwenda masjid kwa sala zake ambapo walimchezea sehemu za siri na kumuharibia udhu ambapo ilimlazimu arudi nyumbani kutia udhu upya na kurejea tena safari ya msikitini.
Photo credit: Globalpublisher.info
more pics after the cut.






No comments:

Post a Comment