Jessica akiendelea kufanya mitihani yake y aform Four akiwa wodini huku wasimamizi wakiwa pembeni yake. |
Jessica akiendelea na mitihani yake kutokea wodini |
MWANAFUNZI
wa kidato cha nne katika Sekondari ya Alfa Germ, Morogoro, Jessica Kiliani
(17), amelazimika kufanya mtihani wake wa kuhitimu elimu hiyo akiwa
wodini baada ya kufanyiwa upasuaji.
Hatua
hiyo ilifikiwa baada ya mwanafunzi huyo, kuomba aruhusiwe kufanya mtihani huo
licha ya kuwa wodini akiugulia maumivu ya upasuaji aliofanyiwa na
madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa zaidi ya saa mbili na kulazwa
katika wodi ya wazazi namba 7B.
No comments:
Post a Comment