Wednesday, February 15, 2012

REDD’S ORIGINAL MDHAMINI MKUU MPYA WA MISS TANZANIA 2012

  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imetangaza rasmi kuchukua nafasi ya “Mdhamini Mkuu” wa shindano kubwa kabisa la urembo hapa nchini lijulikanalo kama “Miss Tanzania”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema; Redds Original, leo inatangaza kuwa ndio wadhamini wakuu wa mashindano ya urembo Tanzania, yanayojulikana kama “Miss Tanzania”. Kwa udhamini huu, mashindano haya sasa yatajulikana kama “REDDS MISS TANZANIA 2012”. Kwa miaka kadhaa sasa Redds Original imekuwa ikishiriki katika mashindano haya kama mdhamini mwenza, yaani “Kinywaji rasmi cha Miss Tanzania”. Hivyo leo tunapiga hatua nyingine kubwa katika historia ya tasnia hii ya urembo hapa nchini kwa kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya Miss Tanzania.
Katika kuonesha kuwa Redds Original, imedhamiria kwa dhati kuendeleza tasnia hii, leo tumesaini mkataba wa udhamini wa mashindano haya kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2014. Hii inawahakikishia wapenzi na mashabiki wa mashindano haya kuwa wataendelea kushuhudia mashindano haya na kuburudika na kinywaji cha Redds Original kwa kipindi chote hiki. Alisema Butallah.
 

 Nae Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Bi. Victoria Kimaro alisisitiza juu ya udhamini wa mashindano haya kuanzia ngazi za chini hadi ngazi ya Taifa. Udhamini huu mkubwa wa mashindano ya Miss Tanzania unajumuisha udhamini tutakaotoa katika maeneo mbali mbali kwa ngazi za vitongoji hadi Taifa. Tunawaahidi mashabiki wote wa mashindano haya na wadau wa tasnia ya urembo kujiandaa kwa burudani ya hali ya juu.
Akizungumzia udhamini huo, Mkurugenzi wa LINO Agency waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Bw. Hasim Lundenga alisema; Kwa niaba ya kamati ya Miss Tanzania napenda kutoa shukurani za dhati kwa TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original kwa udhamini huu, na tunatangaza rasmi kuwa mashindano haya sasa yataitwa “Redds Miss Tanzania’. Kitu kikubwa tunachowashukuru wadhamini wetu ni mkataba ambao tumesaini hii leo, ukituhakikishia udhamini wa mashindano haya kwa miaka mitatu.
Kwa mara nyingine tunawapongeza zaidi Redds original kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia hii ya urembo hapa nchini. Tumekuwa nao bega kwa bega kwa miaka kadhaa sasa, na haiwezekani ukazungumzia tasnia ya urembo hapa nchini bila kuitaja Redds Original. Alisema Lundenga
                                        
Mkurugenzi wa LINO Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania,Hasim Lundenga pamoja na Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Butallah wakisaini mkataba wa makubaliano ya Udhamini kwa kipindi cha miaka mitatu leo jijini Dar es Salaam
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akiongea waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangadha udhamini mkuu wa mashindano ya urembo ya Tanzania (Miss Tanzania) kwa kipindi cha miaka mitatu kupitia kinywaji chake cha Redd's Original.Kulia ni Meneja wa Kinywaji hicho,Victoria Kimaro
Meneja wa Kinywaji  Redd's Original,Victoria Kimaro  akiongea waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangadha udhamini mkuu wa mashindano ya urembo ya Tanzania (Miss Tanzania) kwa kipindi cha miaka mitatu kupitia kinywaji chake cha Redd's Originalwa  kulia kwake ni  Miss Tanzania wa Sasa,Salha Israel
Mkurugenzi wa LINO Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania,Hasim Lundenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akitoa shukrani kwa wadhamini wapya shindano hilo ambao ni Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Redd's Original.Wengine Pichani ni Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Butallah (pili kushoto),Meneja wa Redd's,Victoria Kimaro (wa pili kulia) na Miss Tanzania wa Sasa,Salha Israel
Mdau Albert Makoye ambaye ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania anasema sasa yuko poa na mzigo unaendelea kama kawaida.                                  

No comments:

Post a Comment