Tuesday, March 6, 2012

MASHINDANO YA KUCHOMA NYAMA “SAFARI LAGER NYAMA CHOMA 2012” YATANGAZA BAA ZILIZOFANIKIWA KUINGIA FAINALI DAR ES SALAAM

Jaji mkuu wa mashindano ya Safari Lager Nyama Choma,Douglas Sakibu (katikati) akiongea na waandishi jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza majina ya baa bora zilizochaguliwa kuingia kwenye hatua ya fainali mkoani mbeya baada ya mchujo wa awali.Kushoto ni Mratibu wa Mashindano hayo,Innocent Melleck na Kulia ni Jaji Mkuu Msaidizi wa Mashindano hayo

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza majina ya baa bora zilizochaguliwa kuingia kwenye hatua ya fainali mkoani mbeya baada ya mchujo wa awali kukamilika kwenye yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma 2012”


Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Jijini Dar es Salaam Jaji mkuu wa mashindano hayo Bwana Douglas Sakibu alisema baa zilizochaguliwa kuingia hatua ya fainali jijini Dar es salaam ni Bingwa mtetezi Kisuma Bar,Fyatanga Bar,Play Time Bar,Titanic Bar na Meeda ambazo sasa zinasubiri siku ya fainali kwenye uwanja wa Leaders Club jumapili ya 11/03/2012.

Alisema baa na majiko hayo yatakutana hapo mapema na kufanya shindano la wazi ili kuweza kumpata bingwa wa jiji Dar Es Salaam na wananchi watapata nafasi ya kujionea namna nyama choma inavyoandaliwa katika kiwango cha hali yajuu kabisa.

Baa hizi zilizoingia hatua ya fainali zote zina kiwango cha hali ya juu kabisa na hakika wameonyesha ujuzi na uzoefu mkubwa jambo linaloashiria kuwepo kwa ushindani mkubwa hivyo ni vyema wakazi wa jiji La Dar Es Salaam na vitongoji vyake wakawahi mapema jumapili pale Leaders Club na kupata wasaa wa kushuhudia namna nyama zinavyoandaliwa kwa uhodari mkubwa huku wakiwa na bia yao waipendayo ya Safari Lager.

Kwa upande wake meneja wa bia ya Safari lager ambao ndio waandaaji wa Mashindano hayo Bwana Oscar Shelukindo aliwataka wakazi wa jiji la Dar Es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya fainali na pia mashabiki wa baa hizo kuja kuzishangilia na kuziunga mkono baa zao ili ziweze kuibuka washindi, sambamba na hayo bado kutakuwa na burudani nyingi toka kwenye bendi mbalimbali zitakazotumbuiza siku hiyo ili kuweza kutoa burudani kwa washabiki na wakazi wa jiji hilo kuanzia majira ya saa tano za asubuhi ambapo Burudani zitaongozwa na Bendi maarufu ya Twanga Pepeta , pia kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa washabiki .

Tutaendelea kuwa karibu na wapenzi wetu wa vinywaji toka Tbl hususani wa bia yetu ya Safari kwa kuwapatia burudani mbalimbali,Nyama choma bomba zaidi huku wakipata nafasi ya kujishindia zawadi kibao hivyo ni shindano ambalo mtu hapaswi kukosa hata kidogo.

Wakati huo huo majaji wa mashindano hayo kesho 07/03/2012 wanafanya semina na baa zilizofanikiwa kuchaguliwa jijini Mwanza kisha keshokutwa 08/03/2012 wataanza mchakato rasmi wa kuzitembelea kwenye maeneo yao kwa nyakati tofauti ili kuweza kupata baa zitakazofanikiwa kuingia hatua ya fainali hivi karibuni.

Semina hiyo itashirikisha baa za Cheers pub,Shooters Pub,Mj Bar,Lunala Bar,Shokeni Night Club,HaiInn Bar,If Not Why Not Bar, Friends Conner Bar,Victoria Prince na Ar Pub.

.Alisema hii ni fursa ya pekee kwa wachoma nyama na wenye mabaa kuweza kupata mafunzo yakinifu juu ya uandaaji na uchomaji wa nyama toka kwa wataalam wenye ujuzi na waliobobea kwenye taaluma hiyo ili kuweza kukuza na kuboresha biashara zao na hatimae kufikisha kwa wateja kitu kilichokuwa na ubora wa hali ya juu.

Mashindano ya Safari Nyama Choma mwaka huu yanafanyika kwa mara ya nne ambapo kwa jiji la Mwanza ni mara ya kwanza kufanyika

No comments:

Post a Comment