Friday, May 4, 2012

Yaliyojiri katika birth day ya Mhe Shyrose, Makamanda wa Chadema waikwepa Keki ya Kijani,

 Aaa  Mi sitaki kabisa mambo hayo....Halima mdee akikataa kukata keki ya Shy rose

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi waliangua Vicheko pale wenzao wa CHADEMA walipoikwepa kuigusa nakuila Keki ya Birthday ya Mbunge mteule wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh Shyrose Bhanji wakati wa hafla ya  Hepi Besdei ya kuzaliwa kwake  iliyofanyika usiku wa kuamkia leo  katika ukumbi wa  Nyumbani Lounge, Jijini Dar es Salaam.


Wabunge hao wa CHADEMA  ni Mh.Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum wa chana hicho,  Mh. Lucy Kiwelu picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu. Huku Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Mh Halima Mdee aongoze Ukataji wa Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby Girl Shy Rose Mwwnyewe yenye rangi 'nyutro' kuliwa. Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge wa vyama mbalimbali, wanasiasa, Wasanii wa muziki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake.

Ukiondoa kisa hicho cha Keki, hafla hiyo fupi iliyofana sana, ilionesha jinsi waheshimiwa wabunge wetu walivyo na mshikamano katika jamii, na kudhihirisha ukomavu wa kisiasa kwa kushiriki katika shughuli ya mwenzao bila kujali itikadi zao kisiasa. Na cha kusisimua zaidi ni pale ilipowekwa wazi kwamba mameneja wa kampeni wa Mh Shyrose walikuwa Mh Esther Bulaya (CCM viti maalumu) akisaidiana na Dkt Hamisi Kigwangwala kwa upande wa chama tawala, na Mh Halima Mdee aliyekampenia katika kambi ya upinzani akisaidia na Mh Lucy Kiwelu. Picha na Father Kidevu a.k.a

No comments:

Post a Comment